Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni changamoto:Ban

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza ni changamoto:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka viongozi wa dunia wanaokutana huko Davos, Uswis kwenye mkutano wa biashara kuzidisha nguvu kukabili kasi ya ukuaji wa magonjwa yasiyoambukizwa kwa nchi zinazoendelea ambayo huenda yakaongezeka maradufu hadi kufikia mwaka 2030.

Magonjwa hayo yakiwemo kansa, kiharusi na mshtuko wa moyo yanatajwa kusababisha asilimia 60 ya vifo vyote vinavyotokea.

Ban amesema ulimwengu hauwezi kuziacha nchi maskini zikiendelea kutabika wakati njia na uwezo wa kuzia kutoendelea kukukua kwa magonjwa hayo upo mikononi mwa mataifa mengi yaliyoendelea. Amesema ni jambo la kusikitisha kuona watu zaidi ya milioni 30 hufariki dunia kila mwaka kutokana na magonjwa hayo,na zaidi ya yote nusu ya wanaofariki na watu wenye umri mkubwa kuanzia miaka 70.

Ametaka mataifa yaliyopiga hatua pamoja na Umoja wa Mataifa wenyewe kuweka shabaya ya kufanya kazi kwa karibu na taasisi za uzalishaji madawa ambayo baadaye yatapatikana kwa gharama za chini na kwa kila mwenye uhitaji.