Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Utekaji wa wageni Jamuhuri ya Korea kunatia hofu:UM

Utekaji wa wageni Jamuhuri ya Korea kunatia hofu:UM

Utekaji wa raia wa kigeni wakiwemo wa kutoka Japan nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya watu wa Korea DPRK ni jambo la kutia hofu kwa jumuiya ya kimataifa amesema mtaalamu wa Umoja wa Mataifa nchini DPRK.

Akihitimisha ziara yake nchini Japan Marzuki Darusman ambaye ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu DPRK amesema utekaji nyara huo unauhusiano mkubwa na hali ya haki za binadamu DPRK na ametoa wito kwa wahusika kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Jason Nyakundi anaripoti.