Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Abijan Ivory Coast yakumbwa na Kipindupindu:UNICEF

Abijan Ivory Coast yakumbwa na Kipindupindu:UNICEF

Mlipuko wa kipindupindu katika mji mkuu wa Ivory Coast Abijan umekatili maisha ya watu saba kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF.

Visa 35 vya ugonjwa huo vimearifiwa Abijan na maeneo ya jirani ya Adjame. Mkuu wa UNICEF Ivory Coast Sylvie Dossou amesema mlipuko huo umeua asilimia 20 ya waathirika ambayo ni kubwa. UNICEF na shirika la afya duniani WHO wamepeleka wafanyakazi wake na washirika wengine kusaidia kukabiliana na mlipuko huo.

Mashirika hayo yanagawa vipande vya sabuni 250,000, makasha matano ya kutibu ugonjwa huo yaliyo na dawa za kutibu wagonjwa 1000. Mabango 3000 ya uelimishaji yakimtaka kila mtu kunawa mikono kwa sabuni na kuchagiza usafi pia yamegawanywa.