Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban atoa wito wa mapindunzi ya maendeleo endelevu Duniani

Ban atoa wito wa mapindunzi ya maendeleo endelevu Duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akihutubia kwenye kongamano la kimataifa la uchumi mjini Davos Uswisi amesema ili kuwaondoa watu katika umasikini huku tukilinda mazingira na kuchagiza ukuaji wa uchumi, dunia inahitaji kubadilika.

Amesema mapinduzi yanahitajika katika kufikiri, mtazamo na hatua zinazochukuliwa kuweza kufikia malengo ya kiuchumi na maendeleo duniani.

Ametoa wito wa kufanyika mabadiliko makubwa katika mfumo wa maisha ya watu, katika mikakati ya uchumi, katika masuala ya kijamii na katika maisha ya kisiasa. Pia ametoa wito wa kuvunja ukuta uliopo baina ya ajenda ya maendeleo na ile ya mbadiliko ya hali ya hewa, ukuta baina ya biashara, serikali na jumuiya za kijamii, na usalama wa kimataifa. Amesema ni lazima vyote viende sambamba, biashara nzuri, siasa nzuri na jamii bora.