Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa sotoka ni tishio Korea Kusini:FAO

Ugonjwa wa sotoka ni tishio Korea Kusini:FAO

Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa limewataka madaktari wa mifugo na wale wanaosimamia mipaka barani Asia kuwa macho na kuchunguza wanyama wanaoonyesha dalili za ugongwa wa miguu na midomo kutokana na mkurupuko wa ugonjwa huo nchini Korea Kusini.

Tangu mapema mwezi Novemba mwaka 2010 utawala wa Korea kusini umeweka sheria ya kuzuia usafirishaji wa wanyama na kutoa chanjo inayowalenga nguruwe milioni tisa, ngombe milioni tatu na pia kuwaua mifugo wengine milioni 2.2.

Juan Lubroth, Daktari mkuu katika shirika la FAO anasema kuwa mkurupuko wa ugonjwa huo umekuja kwa kiwango ambacho hakijashuhudiwa kwa nusu karne akisema hali hii inafanya maandalizi kuwa ya juu zaidi. Amesema kuwa Serikali barani Asia lazima zihakikishe kuwa zina uwezo wa kuutambua ugonjwa na kuchukua hatua zinazohitajika