Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafungwa wa kisiasa 2000 washikiliwa Myanmar:UM

Wafungwa wa kisiasa 2000 washikiliwa Myanmar:UM

Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa limeishutumu serikali ya Mynmar kwa kuwazuilia gerezani zaidi ya wafungwa wa kisiasa 2000.

Hata hivyo wanachama wa baraza hilo walikaribisha kuachiliwa kwa mwanasiasa Aung San Suu Kyi ambaye alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani lakini linasema kuwa bado kuna ukiukaji wa haki za binadamu nchini Mynmar ikiwemo dhuluma kwa wafungwa na ubaguzi wa makabila madogo.

Kwa upande wake mwakilishi wa serikali ya Myanmar mjini Geneva Wunna Maung Lwin anasema kuwa mkondo wa miaka saba wa Mynamar kuelekea kwenye demokrasia bado upo baada ya kura ya maoni ya mwaka 2008 na uchaguzi mkuu wa 2010.

Maung Lwin anasema kuwa wanachama wapya wa bunge waliochaguliwa watakutana juma lijalo kuunda serikali mpya akiongeza kuwa hii ndiyo itakuwa awamu ya mwisho kwenye barabara ya demokrasia