Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoa misaada ya kibinadamu wakabiliwa na changamoto Pakistan

Watoa misaada ya kibinadamu wakabiliwa na changamoto Pakistan

Wakati inapowadia miezi sita baada ya mafuriko makubwa kuikumba Pakistan na kusababaisha maafa makubwa bado watoa misaada ya kibanadamu wanaendelea kukabiliwa na changamoto mpya.

Mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya kuisaidia Pakistan Rauf Engin Soysal anasema kuwa baada ya makundi ya kibinadamu kuwasaidia mamilioni ya watu walioathiriwa na mafuriko tangu mwezi Agosti mwaka uliopita kwa sasa ufadhili wa dharura unahitajika.

Anasema kuwa kuna zaidi ya miradi 450 ya kuisadia Pakistan kurejea katika hali ya kawaida akiongeza kuwa ufadahili zaidi unahitajika ili kuiwesesha miradi hii kufanikiwa.