Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi zilizokumbwa na migogoro zisaidiwe:UM

Nchi zilizokumbwa na migogoro zisaidiwe:UM

Nchi ambazo zilikumbwa na migogoro na machafuko ya mara kwa mara lakini sasa zimeanza kuchipua upya zinapaswa kuungwa mkono na kupewa usaidizi wa hali ya juu na jumuiya zote za kimataifa.

Hayo ni mwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamishna ya ujenzi wa amani anayemaliza muda wake balozi Peter Witting wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini New York muda mchache baada ya kukabidhi wadhifa huo kwa kamishna mpya raia wa Rwanda balozi Eugene-Richard Gasana

Balozi Witting amesema kuwa lazima taasisi na mashirika yote ya Umoja wa Mataifa yasaidia juhudi za kuyajenga upya maeneo ambayo yamepitia vipindi vigumu vya machafuko,na isidhaniwe kwamba kazi hiyo ni jukumu la kamishna ya ujenzi wa amani.

Amesema nchi hizo bado zinakabiliwa na changamoto nyingi ambazo utanuzajhi wake unahitaji nguvu ya pamoja kutoka mashirika yote ya Umoja wa Mataifa