Skip to main content

Sudan Kusini wamepiga kura kwa wiki kujitenga:UM

Sudan Kusini wamepiga kura kwa wiki kujitenga:UM

Dalili za awali zinaonyesha kwamba watu wa Sudan Kusini wamepiga kura kwa wingi kuunga mkono kujitenga kutoka Kaskazini na kuwa taifa huru.

Kura ya maoni iliyofanyika tarehe 9 hadi 15 January ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya amani ya CPA ya mwaka 2005 ambayo yalimaliza zaidi ya miongo miwili ya vita baina ya Kaskazini na Kusini. Atul Khare naibu mkuu wa operesheni za kulinda amani za Umoja wa Mataifa ameliambia barazza la usalama kwamba matokeo rasmi yanatarajiwa mwezi february.

Amesema tangu taarifa yake ya mwisho kwenye baraza la usalama tarehe 18 January kura zote za Sudan Kusini zimehesabiwa na ziko katika hatua ya kuhakikiwa na kuidhinishwa. Matokeo ya wali yanatarajiwa kutangazwa tarehe pili .

Kama hakutakuwa na rufaa zozote matokeo rasmi yatatangazwa tarehe 7 Bebruari na endapo kutakuwa na rufaa basi basi yatachukua wiki moja zaidi na kutolewa 14 FebruariDalili za mwanzo kutoka tume ya kura ya maoni ya Sudan Kusini zinaashiria kwamba watu wengi wamepiga kura ya kuunga mkono kujitenga.