Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nategemea serikali mpya Lebanon kutoa ushirikiano:Ban

Nategemea serikali mpya Lebanon kutoa ushirikiano:Ban

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema anatumai kuwa serikali mpya ya Lebanon itatoa ushirikiano wa dhati kwa mahakama maaalumu inayoendesha uchunguzi juu ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Rafiq Hariri aliyeuwawa mwaka 2005.

Mahakama hiyo ambayo inaungwa mkono na Umoja wa Mataifa inazingatia taarifa zilizotolewa na tume moja huru iliyochunguza kisa cha mauwaji hayo.

Serikali ya umoja wa kitaifa iliyoongozwa na Saad Hariri ambaye ni mtoto wa rafiki Hariri, ilivunjika wiki mbili zilizopita, kufuatia mawaziri kadhaa kutoka mafungamano ya Hizbollah kujiuzulu wakipinga serikali hiyo kuiunga mkono mahakama hiyo ya kimataifa.

Taarifa za vyombo vya habari zinasema kuwa rais wa Lebanon Michel Sleiman hii leo amemwomba Najib Mikati ambaye anaungwa mkono na Hizbollah kuunda serikali mpya. Juu ya hilo, Ban ametaka serikali hiyo mpya kutochukua mkondo tofauti na ule wa serikali iliyopita. Amesema ni matumaini yake mahakama hiyo ya kimataifa itapata ushirikiano wa dhati