Skip to main content

Mkuu wa UNHCR aomba dola milioni 280 kusaidia wakimbizi wa Iraq

Mkuu wa UNHCR aomba dola milioni 280 kusaidia wakimbizi wa Iraq

Kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi Antonio Guterres aliyerejea kutoka Iraq amezindua ombi jipya la dola milioni 280 kuwasaidia wakimbizi wa Iraq.

Mipango ya kikanda kwa ajili ya wakimbizi hao inahusisha mashirika 40 ya kimataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanasaidia wakimbizi wa Iraq walioko katika nchi 12 zikiwemo Syria, Jordan, Lebanon, Misri, Uturuki, Iran na mataifa mengine sita ya Ghuba.

Ombi hilo jipya linatanabaisha mahitaji muhimu kwa wakimbizi zaidi ya 190,000 wa Iraq walioorodheshwa na UNHCR katika kanda ya Mashariki ya Kati wengi wao wakiishi Syria na Jordan.