Kuongezaka kwa bei ya chakula kutaathiri pakubwa watu masikini: FAO

Kuongezaka kwa bei ya chakula kutaathiri pakubwa watu masikini: FAO

Bei za chakula duniani zinaongezeka jambo ambalo huenda likasababisha mtafaruku wa chakula kama uliotokea mwaka 2007/2008 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO.

Nchi ambazo ni wazalishaji wakubwa wa chakula wamearifiwa kutaka kuanzisha masharti ya usafirishaji nje bidhaa za kilimo ili kulinda masoko. Lin Sambili na maelezo zaidi.

(SAUTI YA LIN SAMBILI)