Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ahadi pekee hazitoshi kuimarisha afya ya wanawake na watoto asema mkuu wa UM

Ahadi pekee hazitoshi kuimarisha afya ya wanawake na watoto asema mkuu wa UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amerejea msimamo wake wa kuimarisha afya ya wanawake na watoto .

Ban amesema mkakati uliozinduliwa karibuni wa kuimarisha afya ya wanawake na watoto umepata msaada wa fedha wa dola milioni 40. Ameongeza kuwa ingawa fedha ni nyenzo muhimu kwa mkakati huo lazima kuwe na uwajibikaji na uwazi kwa matumizi ya fedha hizo. Katibu Mkuu ameyasema hayo hii leo mjini Geneva wakati wa mkutano wa kwanza wa tume ya uwajibikaji kwa ajili ya afya na wanawake na watoto.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Tume ya uwajibikaji kwa ajili ya afya ya wanawake na watoto ilianzishwa mwaka 2010 kufuatilia msaada kwa ajili ya wanawake na watoto jinsi unavyotumika na endapo matokeo yanayotarajiwa yanapatikana. Mwekiti wa tume hiyo ni Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete na waziri mkuu wa Canada Stephen Harper.