IOM na Lao kupambana na ugonjwa wa TB kwa wahamiaji

25 Januari 2011

Shirika la kimataifa la uhamaiji IOM kwa ushirikiano na wizara ya afya nchini Lao wamezindua mradi wa mwaka mmoja wa kupambana na ugonjwa wa kifua kikuu miongoni mwa jamii ndogo na wahamiaji nchini humo.

Mradi huo ambao utagharimu dola 200,000 unalenga maeneo yaliyo vigumu kufikika nchini Lao chini ya ufadhili wa shirika la kimataifa la maendeleo la Canada, na utawalenga wenyeji wa wilaya kumi zilizo mbali vijijini.

Mwakilishi wa shirika la IOM katika eneo la kusini mashariki mwa Asia Andrew Bruce anasema kuwa umaskini pamoja na mazingira mabaya ya kufanya kazi ni baadhi ya sababu kuu zinazosababisha wahamiaji na watu kutika jamii ndogo kuambukizwa ugonjwa wa kifua kikuu.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter