Kiongozi wa kundi la FDLR la Rwanda afikishwa ICC

25 Januari 2011

Taarifa kutoka mahakama ya kimataifa ya uhalifu ya The Hague zinasema mkuu wa kundi la waasi la Rwanda anayeshutumiwa kuhusika na uhalifu wa kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo amefikishwa kwenye mahakama hiyo hii leo na waendesha mashitaka wa Ufaransa .

Bwana Callixte Mbarushimana alikamatwa mjini Paris mwezi Oktoba mwaka jana kufuatia ombi la mahakama ya ICC. Kiongozi huyo wa waasi wa Kihutu amekana madai kwamba aliamuru wapiganaji wake wa FDLR kuua na kuwabaka raia. Katika majimbo ya Kivu Dr Congo kati ya Januari 20 hadi Februari 25 mwaka 2009.

Bwana Mbarushimana anakabiliwa na makosa matano ya uhalifu dhidi ya ubinadamu na makosa sita ya uhalifu wa kivita ikiwemo mauaji, unyanyasaji, ubakaji, ukatili, matezo na uharibifu wa mali.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud