Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maharamia hawakabiliwi na sheria za kimataifa: UM

Maharamia hawakabiliwi na sheria za kimataifa: UM

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masula ya uharamia Jack Lang amesema kuwa maharamia wengi wa Kisomali wanaaokamatwa kwenye bahari ya Hindi huwa wanaachiliwa bila kufunguliwa mashtaka.

Akiwahutubia waandishi wa habari mjini Washington kabla ya kuwasilisha ripoti kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon kuhusu suala hilo Lang amesema kuwa kutochukuliwa hatua za kisheria dhidi ya maharamia hao kunachangia kuongezeka kwa uharamia. Takriban mabaharia 1200 wametekwa nyara na maharamia mwaka uliopita kwenye bahari ya Hindi. Meli kadha za kivita kutoka sehemu mbali mbali duniani zimekuwa zikipiga doria katika pwani ya Somalia na kwenye Ghuba ya Aden lakini hata hivyo visa vya utekaji nyara wa meli vimetajwa kuongezeka. Hadi sasa washukiwa wa uharamia 700 na wale tayari wamehukumiwa wanazuiliwa kwenye nchi 12 kote duniani huku zaidi ya nusu wakizuiliwa nchini Somalia.