Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati mpya ya kuchunguza mzozo kati ya Israel na Palestina yateuliwa

Kamati mpya ya kuchunguza mzozo kati ya Israel na Palestina yateuliwa

Wanachama wapya wa kamati ya wataalamu wa Umoja wa wanakutana mjini Geneva kanzia hii leo kuamua hatua watakazo chukua na kuimarisha mawasilino na pande zingine.

Kamati hiyo imetwikwa jukumu na baraza la kutetea haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuendelea kuangalia uchunguzi wa ukiukaji wa haki za binadamu kati ya Palestina na Israel wakati wa mzozo wa kati ya Disemba 2008 na Janauri 2009. Kamati hiyo itaongozwa na jaji Mary McGowan Davis ambaye alikuwa mwanachama wa kamati ya zamani pamoja na jaji Lennart Aspegren aliyeteuliwa na mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay kuchukua mahala pa wanachama wawili wanaoondoka. Waatalamu hao wawili wametwikwa jukumu na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuunda ripoti kuhusu jitihada zinazofanya na mataifa ya Palestina na Israel.