Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jamii ya kimataifa yatakiwa kuisadia Somalia:UM

Jamii ya kimataifa yatakiwa kuisadia Somalia:UM

Huku Somalia ikiadhimisha miaka ishirini bila serikali Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa jamii ya kimataifa kujitokeza na kulisaidia taifa hilo lililokumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe linapojikakamia kuwahakikishia amani wananchi wake.

Eneo kubwa la Somalia kwa sasa linakabiliwa na mizozo hali ambayo imechangia zaidi ya watu milioni mbili kuishi katika hali mabaya. Mwezi uliopita Umoja wa Mataifa ulionya kuwa hali ya kiangazi iliyotabiriwa huenda ikawatia mashakani wasomalia zaidi.

Mratibu wa masula ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Mark Bowden anasema kuwa kwa miaka ishirini iliyopita mzozo wa kupigania madaraka, mali na ardhi vimegharimu maisha ya watu na kuwaacha maelfu ya watoto mayatima. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)