Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa UNHCR aikaribisha serikali mpya ya Iraq Baghdad

Mkuu wa UNHCR aikaribisha serikali mpya ya Iraq Baghdad

Kamishina mkuu wa tume ya kuhudumia wakimbizi ya Umoja wa Mataifa UNHCR António Guterres, amesema kuwa serikali mpya ya Iraq inatoa fursa nzuri kwa watu wa nchi hiyo.

Akiongoea baada ya kukamilisha ziara ya siku tatu nchini Iraq Guterres pia alifanya mkutano na na rais wa Iraq Jalal Talabani, waziri mkuu Nouri Al-Maliki pamoja na waziri wa mambo ya kigen Hoshyar Zebari. Guterres amesema kuwa kurejea nyumbani kwa watu kunahitajika kuwa kwa hiari akisema kuwa kuwalizimisha watu kurejea makwao kimyume na matakwa yao na sehemu ambapo hali ya usalama ni mbaya ni jambo ambalo halitakubalika. Kwa sasa kuna raia 196,000 wa Iraq walioooandikishwa kama wakimbizi na shirika la UNHCR nchini Syria , Jordan na Lebanon.UNHCR pia inakadiria kuwa kuna wakimbizi milioni 1.3 wa ndani nchini Iraq wakati 500,000 kati yao wakiishi katika mazingira mabaya.