Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM kuhusu haki za wahamiaji kufanya ziara nchini Afrika Kusini

Mtaalamu wa UM kuhusu haki za wahamiaji kufanya ziara nchini Afrika Kusini

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya haki za wahamiaji Jorge A. Bustamante anatarajiwa kufanya ziara nchini Afrika Kusini ikiwa ndiyo ziara ya kwanza kabisa kama hiyo inayofanywa na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuchunguza na kutoa ripoti kuhusu haki za wahamiaji nchini humo.

Wakati wa ziara yake mjumbe huyo ataangazia masuala kadha yakiwemo uhamiaji wa mara kwa mara , watafuta hifadhi , huduma za afya kwa wahamiaji pamoja na elimu kwa watoto wa wahamaiji.

Kwenye ziara yake ambayo itang'oa nanga tarehe 24 mwezi huu na kukamilika tarehe mosi mwezi ujao wa Februari Mjumbe huyo ataitembelea miji Pretoria , Johannesburg, Polokwane, Musina na Cape Town ambapo atakutana na waakilishji wa serikali , mahakama pamoja na waakilishi wa mashirika ya umma wanaofanya kazi inayohusiana na haki za wahamiaji.