Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mjumbe wa UM Pakistan azuru maneo yaliyoathirika na mafuriko

Mjumbe wa UM Pakistan azuru maneo yaliyoathirika na mafuriko

Takriban miezi sita baada ya mafuriko makubwa kuikumba Pakistan bado Umoja wa Mataifa unafanya jitihada za kuwasaidia mamilioni ya watu wanaohitaji misaada.

Hii ni baada ya ziara ya mjumbe maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na usaidizi kwa Pakistan Rauf Engin Soysal kwenye mkoa wa Sindh ambapo zaidi ya watu milioni saba waliathiriwa na mafuriko hayo. Wakati wa ziara yake Soysal amesema kuwa alifurahishwa na jinsi makundi ya kutoka huduma za kibinadamu yalivyojitahidi kuwasaidia wale wanaohitaji misaada nchini Pakistan. Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na usimaizi wa mikoa na wilaya na mashirika mengine yasiyokuwa ya kiserikali yanatoa misaada ya dharura ambayo inahitajika nchini humo ili kurejea kwa hali ya kawaida.