Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Onyo la kutokea kwa mafuriko latangazwa kusini kwa Afrika

Onyo la kutokea kwa mafuriko latangazwa kusini kwa Afrika

Nchi tano zilizo kwenye kanda ya kusini mwa Afrika zikiwemo Botswana, Musumbiji, Namibia, Zimbabwe and Zambia zimetangaza onyo la kutokea kwa mafuriko kutokana na kiasi kikubwa cha mvua inayoesha katika maeneo hayo.

Kulingana na shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA ni kuwa viwango vya maji kwenye mito ya upper Zambezi and Okavanga ni vya juu zaidi. Huenda maelfu ya watu wakalazimikka kuhama makwao huku malefu ya wengine wakiathirika kutokana na uharibifu wa mimea ya chakula na makao. Huenda pia mafuriko hayo yakasababisha kutokea kwa milipuko ya magonjwa yanayotokana na maji kama vile kipindupindu na pia kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa Malaria. Elizabeth Byrs ni msemaji wa OCHA.

(SAUTI YA ELIZABETH BYRS)