Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mexico yatakiwa kuchunguza hatma ya wahamiaji waliotekwa

Mexico yatakiwa kuchunguza hatma ya wahamiaji waliotekwa

Serikali ya Mexico imetakiwa kuchunguza kisa cha utekaji nyara cha wahamiaji 40 ambao kwa muda wa mwezi mmoja sasa hawajulikani waliko.

Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa wahamiaji hao wengi wao kutoka nchini El Salvador na Guatemala walitekwa nyara katika hali isiyoeleweka wakiwa safarini kwa njia ya gari moshi katika jimbo la Oaxaca kusini mwa Mexico. Pillay anasema kuwa jitihada za kuwapata wahamiaji hao hazijazaa matunda na wanaharakati wa haki za binadamu ambao wamekuwa wakishughulikia suala hilo wamekuwa wakipokea vitisho vya kuuawa. Rupert Colville ni msemaji katika afisi ya ya tume ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)

Tume hiyo pia imeelezea kusikitishwa kwake kuhusiana na kuendelea kuzorota kwa haki za wahamiaji nchini Mexico ikisema kuwa maelfun ya wahamiaji wametekwa nyara kwa muda wa miaka miwili iliyopita.