Chanjo dhidi ya homa ya manjano kuanza nchini Ivory Coast
Chanjo ya siku saba dhidi ya homa ya manjano inatarajiwa kuanza hapo kwesho nchini Ivory Coast ikiwalenga zaidi ya watu 830,000 wakiwemo watu wazima na watoto kwenye wilaya nne walio na umri wa miezi tisa na zaidi.
Afisa anayesimamia afisi ya shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF nchini Ivory Coast Sylvie Dossou aliyashukuru mashirika yaliyoungana kutoa chanjo hiyo . Amesema kuwa kampeni hiyo inaonyesha ulimwengyu kuwa hata kama kuna mzozo wa kisiasa nchini Ivory Coast huduma za kibinadamu za kuokoa maisha bado zinaendelera.