Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Ivory Coast wasirejeshwe:UNHCR

Wakimbizi wa Ivory Coast wasirejeshwe:UNHCR

Shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Maataifa UNHCR limetoa wito kwa serikali kote duniani kukoma kuwarejesha makwao wakimbizi au wahamiaji kutoka Ivory Coast.

UNHCR inasema kuwa hali ya usalama nchini Ivory Coast sio salama kuruhusu kurejea nyumbani wahamiaji au wakimbizi hao. Msemaji wa UNHCR mjini Geneva Andrej Mahecic anasema kuwa shirika hilo limekaribisha hatua za Liberia na Guinea kwa kuwakubali wale wanaokimbia ghasia nchini Ivory Coast kama wakimbizi. UNHCR inasema kuwa zaidi ya wakimbizi 30,000 kutoka Ivory Coast wamekimbilia Liberia huku wengine 18,000 wakiiwa wakimbizi wa ndani katika maneo mbali mbali magharibi mwa nchi.