Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM kuendelea kufadhili maendeleo kwenye nchi za Kiarabu:Ban

UM kuendelea kufadhili maendeleo kwenye nchi za Kiarabu:Ban

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesema kuwa shirika hilo liko tayari kusaidia nchi za kiarabu na washirika wao kutimiza malengo yao ya kiuchumi kama moja ya njia moja ya kuweka msingi bora wa amani katika siku zijazo.

Kupitia ujumbe uliosomwa kwa niaba yake kwenye mkutano wa pili wa nchi za kiarabu kuhusu maendeleo ya kijaamii na kiuchumi kwenye mji wa Sharm El-Sheikh nchini Misri Ban amesema kuwa kwa kuungana pamoja maisha ya akina yanaweza kuboreshwa na kutoa fursa znyingi kwa vijana.

Ban amesema kuwa mataifa ya kiarabu yamepiga hatua katika kutimiza malengo ya millennia lakini hata hivyo manufaa yake hayalingani miongoni mwa mataifa hayo. Katibu mkuu ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa upatikanaji wa nafasi za ajira unaenda sambamba na kasi ya kuongezeka kwa watu.