Skip to main content

Ban amteua mwakilishi mpya wa UM Guinea-Bissau

Ban amteua mwakilishi mpya wa UM Guinea-Bissau

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amemteuwa Gana Fofang wa Cameroon kuwa naibu mwakilishi mpya wa Umoja wa Mataifa nchini Guinea-Bissau.

Bwana Fofang atakuwa pia mratibu wa masuala ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo UNDP katika nchi hiyo ya Afrika ya Magharibi.

Fofan amefanya kazi katika mfumo wa Umoj wa Mataifa kwa muda mrefu katika Nyanja za maendeleo baada ya migogoro, kusaidia masuala ya uchaguzi, masuala ya mabadiliko ya mifumo ya madini, masuala ya kisheria na sekta ya ulinzi, siasa, uchumi na utawala bora.

Kwa sasa Fofang ni mrtibu wa Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa UNDP katika kisiwa cha Sao Tome na Principe, na kabla ya hapo alikuwa mshauri wa sera wa UNDP Afrika na mradi wa milenia New york kuanzia 2006 hadi 2008. Na ameshawahi kuwa mwakilishi wa UNDP Laos, Rwanda na Msumbiji.