Filamu ya usafirishaji haramu watoto yaonyeshwa:UNICEF

20 Januari 2011

Filamu fupi iitwayo "not my life" yaani sio maisha yangu inayohusu unyonyaji na ukatili wa watoto imeanza kuonyeshwa jana kwenye kituo cha lincolin hapa New York.

Filamu hiyo iliyorekodiwa katika mabara matano duniani inaangalia masuala ya usafirishaji haramu wa watoto, kutimiwa kama watumwa wa ngono na utumikishwaji haramu wa watoto.

Filamu ya not my life imemshirikisha mkurugenzi wa mipango wa shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF Dr Nicholas Alipui na dr Susan Bissell wa UNICEF mkuu wa masuala ya kuwalinda watoto wanaoelezea masuala muhimu kuhusu haki za watoto. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter