Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwaka 2010 ilighubikwa na joto sana katika historia: WMO

Mwaka 2010 ilighubikwa na joto sana katika historia: WMO

Kwa mujibu wa shirika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO mwaka 2010 ni mwaka ulioweka rekodi ya kuwa na joto sana sambamba na ule wa 2005 na 1998.

Takwimu zilizoifikiwa WMO zinaonyesha hakuna hakuna tofauti ya kiwango cha choto duniani kwa mwaka 2010, 2005 na 1998.  Mwaka 2010 wastani wa joto la dunia ulikuwa nyuzi joto 0.53C kikiwa ni kiwango cha juu ikilinganishwa na mwaka 1961 hadi 1990, na kilikuwa nyuzi joto 0.01 zaidi ya kile cha 2005 na nyuzi joto 0.02 zaidi ya kile cha 1998. Michel Jarraud ni katibu mkuu wa WMO anasema takwimu za 2010 zinathibitisha mfumo wa muda mrefu wa ongezeko la joto duniani.

(SAUTI YA MICHEL JARRAUD)

Ameongeza kuwa katika kipindi cha miaka 10 tangu 2001 hadi 2010 kiwango cha wastani cha joto duniani kimekuwa nyuzi joto 0.46 C kikiwa cha juu zaidi ya kile cha 1961 na ni kikubwa zaidi kuwahi kurekodiwa katika muda wa miaka 10 tangu kuanza kuhifadhiwa takwimu. Na hivi karibuni joto kubwa limearifiwa Afrika, baadhi ya sehemu za Asia na baadhi ya sehemu za Arctic.