DR Congo, Uganda na MONUSCO wako katika mpango wa kuwafurusha waasi wa Uganda wa ADF/NALU

19 Januari 2011

Operesheni ya pamoja ya jeshi la taifa la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Uganda na mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani Congo MONUSCO awamu ya nne imeanza mwishoni mwa wiki kuwasaka waasi wa Uganda wa ADF/NALU na makundi mengine ya yenye silaha Mashariki mwa Congo.

Opreresheni hii ni ya awamu ya nne baada ya zile zilizoanza katikati ya mwaka jana katika mistu iliyoko chini yam lima Ruwenzori upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo jimbo la Kivu ya Kaskazini.

Mwandihi habari mjini Beni Mseke Dide amezungumza na Meja Celestine Ngeleka afisa wa usimamizi na mawasiliano wa operesheni hiyo kutoka jeshi la serikali ya Congo ili kupata ufafanuzi wa operesheni hiyo Mashariki mwa Congo.

(MAHOJIANO NA MEJA CELESTINE)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter