Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban kuhudhuria mikutano Switzerland na Ethiopia wiki ijayo

Ban kuhudhuria mikutano Switzerland na Ethiopia wiki ijayo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon anatazamiwa kuanza ziara ya kuzitembelea nchi za Switzerland na Ethiopia wiki ijayo ambako atakuwa na mikutano kadhaa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wake, Ban akiwa nchini Switzerland atafungua mkutano ambao umeandaliwa na shirika la usamaria wema OCHA,kwa ajili ya kutunisha mfuko wake wa fedha. Pia atahudhuria tukio muhimu la kila mwaka litakalowaleta pamoja wadau wanaojishughulisha na misaada ya usamaria mwema.

Kadhalika huko Geneva,Katibu Mkuu huyo atahutubia baraza la Haki za binadamu pamoja na mikutano mingine kadhaa ya kimataifa. Baada ya hapo anatazamiwa kusafiri hadi Addis Ababa, Ethiopia, ambako atahudhuria mkutano wa 16 wa Umoja wa Afrika na kukutana na viongozi kadhaa.