Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

OCHA yatenga dola milioni 84kuwasaidia wenye matatizo

OCHA yatenga dola milioni 84kuwasaidia wenye matatizo

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya usamaria mwema, limetenga kiasi cha dola za kimarekani milioni 84 kwa ajili ya kuwafikia watu wenye kuhitaji manitaji ya dharura ambao bado hawajatupiwa jicho.

Inakadiriwa kwamba mamia kwa maelfu ya watu duniani kote wanaendelea kutaabika kutokana na shida mbalimbali ikiwemo zile zinazosababishwa na ukosefu wa chakula, utapiamlo, magonjwa pamoja na mikwamo ya kisiasa.

Mratibu wa shirika hilo la Umoja wa mataifa Valerie Amos amesema kuwa nchi 15 zinatazamiwa kufikiwa na fedha hizo ambazo zimetolewa na mfuko maalumu ulioundwa hivi karibuni kwa ajili ya kuyakabili majanga ya dharura CERF.

Hii ni mara ya kwanza kwa mfuko huo kutoa kiasi kikubwa cha fedha tangu kuanzishwa kwake na fungu jingine la fedha huenda likaidhinishwa mwezi July mwaka huu. Wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada ya kiutu nchini Somalia wanatazamiwa kupatiwa kiasi kikubwa cha fedha kinachofikia dola milioni 11.