Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ombi la Dola milioni 51 kuwasaidia Wasri Lanka latolewa

Ombi la Dola milioni 51 kuwasaidia Wasri Lanka latolewa

Umoja wa Mataifa na washirika wake wamezindua ombi la msaada wa dola milioni 51 kuisaidia serikali ya Sri Lanka kushughulikia mahitaji ya zaidi ya watu milioni moja walioathirika na mafuriko kwa miezi sita ijayo.

Ombi hilo litapitiwa tena mwezi ujao kuangalia upya mahitaji ya watu baada ya matokeo ya tathimini ya kina.Sri Lanka imeshuhudia mvua kubwa kuwahi kunyesha katika takribani miaka 100. Mvua hizo zilianza Desemba 26 mwaka 2010 na kusababisha mafuriko na maporomoko ya udongo nchini humo. Maeneo yaliyoathirika zaidi na mafuriko hayo ni mji mkuu Colombo na wilaya za Kaskazini hali inayowaweka maelfu ya wakimbizi wanaorejea katika mazingira magumu.