Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu zaidi ya 100 wafa Tunisia, UM kupeleka timu

Watu zaidi ya 100 wafa Tunisia, UM kupeleka timu

Kamishina mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu Navi Pillay leo amesema watu zaidi ya 100 wamekufa katika machafuko yanayoendelea nchini Tunisia na anapanga kupeleka timu kutathimini hali nchini humo katika siku chahce zijazo.

Katika taarifa maalumu aliyoitoa mjini Geneva Bi Pillay amesema ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu umekuwa kitovu cha matatizo Tunisia na hivyo haki za binadamu ni lazima ziwekwe mbele katika kusuluhisha matatizo hayo.

Ameongeza kwamba anatarajia timu yake pamoja na kukusanya taarifa ya ukiukaji wa haki za binadamu siku za nyuma na sasa , itarejea na mapendekezo ya hatua za kuchukua kushughulikia masuala ya siku za nyuma na mabadiliko ya siku za usoni.

(SAUTI NAVI PILLAY)