Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mvutano wa kisiasa nchini Ivory Coast bado uko njia panda

Mvutano wa kisiasa nchini Ivory Coast bado uko njia panda

Mvutano wa kisiasa nchini Ivory Coast bado uko njia panda baada ya mjumbe wa muungano wa Afrika aliyekwenda kutafuta suluhu ya mzozo juhudi zake kushindwa kuzaa matunda.

Raila Odinga ambaye ni waziri mkuu wa Kenya ametazangaza kwamba ameshindwa kupata suluhu katika juhudi zake za upatanishi kumaliza mvutano baina ya Laurent Gbagbo na Alassane Ouatarra nchini Ivory Coast.

Akiondoka nchini humo ameonya kwamba muda unakimbia na amemshutumu bwana Gbagbo kwa kuvunja ahadi yake ya kuondoa vizuizi kwenye hotel ya Gulf ambayo inatumika kama makao makuu ya Alassane Ouattar na washirika wake.

Sasa juhudi zitakazofuata za mjumbe huyo wa muungano wa Afrika bwana Odinga ni mashauriano na nchi za Ghana, Angola na Burkina Faso. Maelfu ya watu wanaendelea kukimbia nchini humo huku kukiripotiwa ufyatuliwaji wa risasi katika eneo la Abobo anakoungwa mkono bwana Ouatarra na mtu mmoja inasemekana ameuawawa na polisi.