Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya watu milioni 1.1 wameathirika na mafuriko Sri Lanka

Zaidi ya watu milioni 1.1 wameathirika na mafuriko Sri Lanka

Zaidi ya watu milioni 1.1 walioathirika na mafuriko nchini Sri Lanka sasa wanapata msaada kutoka mashirika ya misaada ya kibinadamu yaliyoko nchini humo.

Baadaye wiki hii shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA litazindua ombi la fedha ili kuongeza msaada kwa waathirika. Wakati huohuo shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limetoa fedha kusaidia vifaa ambavyo si chakula kwa familia takribani 3000 Mashariki mwa Sri Lanka.

Jemini Pandya msemaji wa IOM mjini Geneva anasema zaidi ya watu 58,000 hivi sasa wanapata hifadhi katika kambi za wakimbizi wa ndani katika wilya za Batticaloa, Trincomalee na Ampara Mashariki mwa nchi hiyo.

Ameongeza kuwa IOM imeoombwa na serikali na Umoja wa Mataifa kuratibu kazi za mashirika ya misaada, kuwasaidia watu takriban milioni 1.1 kwa malazi na vitu muhimu visivyo chakula.