Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Matokeo ya kura ya maoni Sudan yanakusanywa:Mkapa

Matokeo ya kura ya maoni Sudan yanakusanywa:Mkapa

Matokeo ya kura ya maoni ya kujitenga ama la kwa Sudan Kusini yanakusanywa pamoja hivi sasa kutoka vituo 3000 .

Jopo la Umoja wa Mataifa la kuangalia mchakato wa kura hiyo limesema hadi hivi sasa halijaona ushahidi wowote wa kuonyesha kwamba kulikuwa na jaribio au njma za kufanya udanganyifu kwenye kura hiyo.

Mkuu wa jopo hilo Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa, anasema kwa sasa wanafuatilia kwa karibu ukusanyaji wa wa matokeo.

Mchakato wa kusafirisha matokeo kutoka vituo karibu 3000 vya kura ya maoni kuyapeleka kwenye kamati ndogo zilizoandaliwa na kisha Juba na hatimaye Khartoum. Tunafahamu kwamba madai yoyote ya makosa au udanganyifu yatachunguzwa kwa kina na matokeo yoyote yatakayokuwa ni ya kimakosa yatashughulikiwa ipasavyo.

Bwana Mkapa amesisitiza kwamba matokeo ya kura hiyo ya maoni ili iwe ya mafanikio ni lazima Sudan Kusini na Kaskazini watatue masuala mengine muhimu baina yao baada ya kura hiyo.