Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sekta ya utalii iliimarika 2010:UNWTO

Sekta ya utalii iliimarika 2010:UNWTO

Shirika la utalii la Umoja wa Mataifa UNWTO linasema kuwa sekta ya utalii ilishuhudia mafanikio makubwa mwaka uliopita baada ya kudorora kutokana na hali mbaya ya uchumi iliyoikumba dunia mwaka 2008 na 2009.

Shirika hilo linasema kuwa maeneo mengi yalishuhudia idai kubwa ya watalii lakini hata hivyo ni nchi zinazoendelea ndizo zinafaidika zaidi. Mkurugenzi wa shirika la UNWTO Taleb Rifai amesema kuwa kuboreka kwa sekta ya utalii ni mafanikio kwa nchi zinazoendelea zinazotegemea sekta hiyo.

Amesema kuwa kwa sasa changamoto iliyopo ni kuendeleza hali hii katika miaka ijayo. Hata hivyo ukuaji wa sekta ya utalii barani ulaya na maeneo mengine ulikuwa wa chini hususan kutokana na matatizo ya usafiri yaliyosababishwa na kulipuka kwa milima ya volcano nchini Iceland.