Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yatiwa moyo na hatua za kusaidia wakimbizi Yemen

UNHCR yatiwa moyo na hatua za kusaidia wakimbizi Yemen

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limetiwa moyo na mikutano yenye matunda iliyofanyika siku chache zilizopita baina ya uongozi wa seriikali na wawakilishi wa al-Houthi kuhusu haja ya kuboresha msaada wa kibinadamu Kaskazini mwa nchi hiyo.

Hatua hiyo imefuatia ziara ya kamisha mkuu wa UNHCR bwana Antonio guterres nchini humo. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Hii ndiyo ziara ya kwanza ya maafisa wa ngazi za juu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la Sa'ada tangu kutokea kwa mzozo wa hivi majuzi kati ya mwezi Agosti na Februari mwaka uliopita. Hali yenye utata pamoja na kujikokota katika kupatikana kwa makubaliano ya amani vimetatiza kurejea nyumbani idadi kubwa ya watu waliolazimika kukimbia makwao.

Hali hiyo pia inaamaanisha kuwa hakuna usambazaji mkubwa wa misaada katika maeneo ya mkoa wa Sa'ada. Huku watu waliokimbia makwao wakilazimika kujitafutia chakula mwaka mmoja baada ya kutiwa sahihi makubalino ya kusitisha mapigano.

Zaidi ya wakimbizi wa ndani 300,000 waliolazimika kuhama makwao wakati wa mizozo kati ya serikali na vikosi vya kundi la al-Houthi tangu mwaka 2004 ni wakimbizi 20,000 waliofanikiwa kurejea nyumbani hadi leo.