UNHCR yahofia Sweden kuwarejesha wakimbizi wa Iraq

18 Januari 2011

Sweden inampango wa kuwarejesha kwa nguvu Baghdad siku ya Jumatano wiki hii wakimbizi 25 wa Iaq, hatua ambayo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR linasema itakuwa inakiuka mkataba wa wakimbizi.

UNHCR inasema watu ambao watarejeshwa walikuwa ni waomba hifadhi ambao wanastahili kulindwa chini ya mkataba wa wakimbizi wa mwaka 1951 au sheria za muungano wa Ulaya zinazosema kuwalinda watu wanaohitaji ulinzi kama wanatoka kwenye makundi ya kikabila au kidini yanayoengwa na ghasia nchini Iraq. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(SAUTI YA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter