Mabadiliko kwenye baraza la usalama kuanza 2011:Deiss

Mabadiliko kwenye baraza la usalama kuanza 2011:Deiss

Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Joseph Deiss leo amesema ina matumaini kwamba mazungumzo hasa ya kupanua wigo wa baraza la usalama yanaweza kuanza mwaka huu.

Hatua hiyo itakuwa ni baada ya karibu miongo miwili ya mchakato wa kutaka kuongeza viti vya babaraza hilo, ambalo hadi sasa maamuzi yake ynategemea wajumbe 15 waliopo.

Mara ya mwisho baraza hilo liliongeza wajumbe mwaka 1965 kutoka wajumbe 11 wakiwemo 5 wa kudumu ambao ni Ufaransa, Urusi, Marekani, uingereza na Uchina hadi wajumbe 15 wakati ambao Umoja wa Mataifa ulikuwa na nchi wanachama 118 tuu.

Leo hii Umoja wa Mataifa una wajumbe 192, lakini jaribio katika miaka 18 iliyopita ya kuongeza wajumbe wa baraza hilo yamekuwa yakikabiliwa na vizingiti kikiwemo cha wajumbe wangapi waongezwe, endapo vingine view vya kudumu na endapo vitakuwa uwezo wa kura ya turufu au la.

Kwa sasa wajumbe 10 ambao sio wa kudumu wanachaguliwa kwa muhula wa miaka miwili miwili na hawana kura ya turufu. Kundi linaloitwa G4 likijumuisha Ujerumani, Brazil, India na Japan wanafikiriwa kama wanaweza kuwa wajumbe wa kudumu wakati Afrika pia inataka wajumbe wawili wa kudumu.