Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkurugenzi wa WFP ziarani Mashariki ya Kati

Mkurugenzi wa WFP ziarani Mashariki ya Kati

Mkurugenzi wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP Josette Sheeran hii leo ataanza ziara ya siku tatu katika ardhi iliyotawaliwa ya palestina ambapo pia atafanya ziara nchini Israel na Jordan na kutembelea miradi ya shirika la WFP kufanya mikutano na maafisa wa serikali , washirika wake na wafanyikazi wa WFP.

Sheeran atazuru miradi ya chakula shuleni ikiwemo miradi ya kulisha watoto kwa njia ya elektroniki katika eneo la ukingo wa magharibi. Pia atazuru shule ya zamani zaidi katika eneo la Hebron na kukutana na wanafunzi na kuona athari na mradi huo kwa maisha ya wanafunzi. Zaidi ya wanafunzi 75,000 huwa wanapokea chakula shuleni kutoka kwa shirika la WFP katika eneo la ukingo wa magharibi. Lin Sambili na taarifa kamili

(SAUTI YA LIN SAMBILI)