Skip to main content

Ban atoa wito kukabili changamoto za nishati

Ban atoa wito kukabili changamoto za nishati

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amesisitiza kuwepo kwa mabadiliko kwenye nguvu ya nishati akisema kuwa ulimwengu wa sasa unahitaji mabadiliko kwenda kwa kawi iliyo safi mabadiliko ambayo yatamwesesha kila mmoja kupata kawi iliyo nafuu.

Ban ambaye yuko ziarani katika nchi za falme za Kiarabu akitoa mfano ya jitihada zinazofanywa ili kupatikana kwa nishati iliyo safi kote duniani Ban amesema kuwa siku nzuri za baadaye ziko njiani.
Katika miaka ishirini ijayo matumizi ya nishati yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 40 wakati tayari watu bilioni 1.6 hawana umeme kwenye nchi zinazoendelea huku watu bilioni tatu wakitegemea nishati za kitamaduni kwa kupika na matumizi mengine ya nyumbani.