Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaanza kuwasaidia wakimbizi wa Ivory Coast

IOM yaanza kuwasaidia wakimbizi wa Ivory Coast

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limenza kuwasajili wakimbizi wa ndani magharibi kwa Ivory Coast huku wafanyikazi wa shirika hilo wakipiga kambi katika eneo hilo kutoa misaada ya mahema.

Kundi la takriban watu 16,000 waliolazimika kukimbia makwao kufutia ghasia za baada ya uchaguzi wamepiga kambi katika maeneo ya Danané, Duékoué na Man, magharibi mwa Ivory Coast wakati idadi kubwa ikiwajumuisha wanawake na watoto. Mashirika kadha kwa sasa yanafanya jitihada za kutoa misaada ya kibinadamu likiwemo shirika la IOM. Misaada kutoka kwa shirika hilo pia inatarajiwa kupelekewa wakimbizi siku chache zijazo.

(SAUTI YA JEAN PHILIPPE CHAUZY)

Hapo kesho IOM itasafirisha kundi la wakimbizi 52 wa Ivory Coast kwenda kwa kambi ya wakimbizi nchini Guinea kufuatia ombi lililotolewa na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR . Pia juma lililopita IOM ilisaidia katika kuwasafirisha wakimbizi elfu 82.