Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jumuiya ya kimataifa isaidie vikosi vya AMISOM Somalia:UM

Jumuiya ya kimataifa isaidie vikosi vya AMISOM Somalia:UM

Umoja wa Mataifa umepaza sauti yake ukitaja jumuiya za kimataifa kuvisaidia vikosi vya kulinda amani nchini Somalia ambavyo vinakabiliwa na mbinyo toka kwa kundi la kigaida la Al-Shabaab ambalo linapaambana kuudhibiti mji mkuu wa Mogadishu.

Vikosi hivyo vya umoja wa afrika AMISOM vimekuwa kwenye wakati mgumu kutimiza majukumu yake kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya kifedha na vitendea kazi.

Mwakilishi wa Katibu Mkuu nchini Somalia Augustine Mahiga ametaka jumuiya ya kimataifa kutoa misaada zaidi ikiwemo uchangiaji wa fedha na kuongeza idadi ya askari kutoka 8,000 waliopo sasa hadi kufikia 12,000 ili utendaji kazi wa vikosi hivyo uweze kuzaa matunda ya haraka.

Mji mkuu wa Mogadishu umekuwa kitovu muhimu cha mapigano. Pande zote mbili zinaelekeza shabaya yao kwenye mji huo kila upande ukitaka kuweka kwenye himaya yake.