UNAMID yaashiria mtazamo imara zaidi Darfur:Gambari

UNAMID yaashiria mtazamo imara zaidi Darfur:Gambari

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na muungano wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID umeitahadharisha serikali ya Sudan kwamba itachukua mtazamo imara zaidi katika kutekeleza majukumu yake mwaka huu.

Jukumu la UNAMID katika jimbo la Darfur ni kusaidia upatikanaji wa misaada ya kibinadamu na kuwalinda raia. Ibrahim Gambari, mwakilishi maalumu wa UNAMID anasema kazi ya walinda amani isizuwiliwe.

Anasema wakati mwingine tumezuiliwa kutimiza wajibu wetu.

Tutakuwa imara zaidi, pia tunatoa ishara kwa serikali kwamba hatutokuwa tukitaka rukhusa ya kutimiza wajibu wetu kwa sababu makubaliano yetu yanatuwezesha kutembea na kufanya kazi kwa uhuru . Na tutafanya hivyo.