Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mchakato wa kura ya maoni Sudan unaenda vizuri:Mkapa

Mchakato wa kura ya maoni Sudan unaenda vizuri:Mkapa

Jopo la Umoja wa Mataifa linaloangalia kura ya maoni ya kihistoria nchini Sudan linasema ikiwa imesalia siku moja tuu ya upigaji kura kuamua hatma ya taifa hilo mchakato mzima umekwenda shwari.

Jopo hilo linaloongozwa na Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa limepata fursa ya kutembelea vituo mbalimbali vya kupigia kura katika majimbo ya Kusini na pia Kaskazini kukutana na wapiga kura, wasimamizi wa vituo na uongozi wa maeneo hayo.

Mwenyekiti Bwana mkapa anasema kura hiyo iliyoanza Januari 9 na iliyopangwa kukamilika jumamosi Januari 15 haikukumbwa na matatizo yoyote makubwa na jopo hilo limedhirisha na mchakato mzima.

(SAUTI YA BENJAMIN MKAPA)

Ameongeza kuwa Wasudan Kusini takriban milioni nne walioajiandikisha wanatarajiwa kukamilisha zoezi hilo hapo kesho na matokeo ya awali yanatarajiwa kati ya tarehe 21 na 27 ya mwezi huu na tume ya kura ya maoni ndio itakayotangaza matokeo rasmi baada ya kuhakikiwa.