Ujumbe wa UM na muungano wa Afrika wazuru Niger kutathmini hali ya mambo

14 Januari 2011

Muungano wa tume ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika umewasili nchini Niger kwa ajili ya kuhakiki hatua zilizopigwa na serikali ya mpito ambayo ilitwaa madaraka mwaka uliopita baada ya kufanya mapinduzi.

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu katika nchi za Afrika Magharibi, Said Djinnit ameongoza msafara huo akiwa amefuatana na Kamishna mmoja kutoka Umoja wa Afrika Ramtane Lamamra na Makamu Rais wa Jumuiya ya kiuchumi ya afrika magharibi ECOWAS Jean de Dieu Somba.

Ujumbe huo unafuatilia hatua zinazoendelea kuchukuliwa na serikali ya mpito ili kurejesha nchi hiyo kwenye utulivu wa kawaida pamoja na kutathmini uwezekano wa kufanyika uchaguzi wa kidemokrasia. Wakiwa nchini humo wanadiplomasia hao watakutana na watu wa makundi mbalimbali ikiwemo pia wagombea wa nafasi ya urais.

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter