Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu 247 wauawa kufuatia mzozo wa kisiasa Ivory Coast:UM

Watu 247 wauawa kufuatia mzozo wa kisiasa Ivory Coast:UM

Tume ya kutetea haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa idadi ya watu waliouawa nchini Ivory kufuatia kuzuka kwa mzozo wa kisiasa imeongezeka na kufikia 247 .

Msemaji wa tumre hiyo Rupert Colville anasema kuwa waliouawa wanatoka pande zote mbili zinazopingana na kuongeza kuwa hata hivyo hakuna dhibitisho la kuwepo kwa makaburi ya pamoja.

Hata hivyo amesema kuwa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI kimepokea ripoti za kuwepo kwa makaburi hayo ya pamoja lakini jitihada na kudhibitisha madai hayo zimetatizwa na wanajeshi.

(SAUTI YA RUPERT COLVILE)

Umoja wa Mataifa unasema kuwa umepokea takriban visa 49 vya kutoweka kwa watu. Ivory Coast imekuwa kwenye mzozo tangu uchaguzi wa tarehe 29 mwezi Novemba mwaka uliopita ambao jamii ya kimataifa inaamini ulishindwa na Alassane Ouattara.