Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mzozo wa kisiasa waibuka tena ndani ya serikali ya Somalia

Mzozo wa kisiasa waibuka tena ndani ya serikali ya Somalia

Mzozo mpya wa kisiasa umeibuka ndani ya serikali ya mpito ya Somalia katia ya rais na spika wa bunge kuhusu serikalia ya mpito ambayo kuhudumu kwake kunatarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.

Inaarifiwa kuwa mzozo huo uliibuka baada ya rais Sheikh Sharif Ahmed kumtaka spika wa bunge Sharif Hassan Sheikh Aden kukamilisha uteuzi wa wabunge wapya. Hata hivyo ripoti zinasema kuwa spika Sharif Hassan amekataa kuwaapisha wabunge akisema kuwa badala yake kutaundwa katiba mpya na kufuatiwa na uchaguzi mpya wa urais.

Uamuzi huo wa spika unaonekana kumtatiza rais Sharif baada ya kile kinachodaiwa na wataalamu kuwa mipango yake ya kutaka kuongezewa muda wa kuhudumu kama rais . Inadaiwa kuwa rais Sharif anataka nafasi za wabunge 200 zilizosalia kujazwa na wafuasi wake ili bunge liweze kupitisha kura ya kumwongezea muda.